Menu
 Na Ezekiel Kamanga.
Raia wa nchi ya Somalia  Mohamed Ahmed (31) anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumbaka mtoto  mweye umri wa miaka miwili jina limehifadhiwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema kuwa  lilitokea jumapili ya pasaka majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Kambi katoto wilayani Chunya.

Alisema kuwa Mtuhumiwa Ahmed akiwa na nia ovu alimchukua mtoto nyumbani kwao na kisha kwenda kumbaka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

“Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alienda kumchukua mtoto nyumbani kwao na kwenda nae sehemu isiyojulikana kisha kumbaka, bado tunafanya upepelezi ikithibitika ni kweli mtuhumiwa amehusika tutamfikisha mahakani kwa ajili ya hatua zaidi”alisema.

Katika tukio jingine alisema Mwanamke, Mwanashija Teru aliuwawa na watu wasiofahamika baada ya kukatwa na kitu chenye kali sehemu mbalimbali za mwili wake usiku wakati akiwa amelala.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 23 mwaka huu eneo la Kipambawe wilayani Chunya na kuripotiwa polisi Jumapili ya pasaka kutokana na umbali mrefu uliopo kati ya kituo cha polisi na eneo la tukio.

“Mwanamke huyo alikatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani, Shingoni na mikononi wakati akiwa amelala usiku wa manane na watu wasiofahamika kwa hiyo tu nachunguza tukio hilo pamoja na kuwasaka wahusika ili wafikishwe mahakamani.”alisema
 
Top