Menu
 


Chiku Gallawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Luteni Mstaafu Chiku Gallawa baada ya kumuapisha kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
Na Ezekiel Kamanga, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luten Mstaafu Chiku Galawa ameanza ziara ya kutembelea Wilaya zote tano za Mbozi Songwe,Ileje,Momba na Songwe ambazo zinaunda Mkoa wa Songwe ili kujitambulisha kwa wananchi na kupokea changamoto mbalimbali zinazozikabili wilaya hizo.

Galawa ameanza ziara katika Wilaya ya Songwe ambapo alipokelewa katika Kijiji cha Kaloleni Kata ya Mkwajuni na Vijana waendesha Bodaboda walioambatana na Mbunge wa Jimbo la Songwe Philip Mulugo ambaye ni mlezi wa Vikundi mbalimbali vya waendesha pikipiki Wilaya ya Songwe.

Mkuu wa Mkoa Chiku Galawa alipokea changamoto mbalimbali za Jimbo la Songwe kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ikiwa ni pamoja maji,barabara,umeme na Afya.

Mulugo amesema kuwa wilaya hiyo mpya ina eneo la kutosha kujenga nyumba za watumishi wa wilaya hiyo na ofisi mbalimbali pia Asasi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Benki ya NMB ili kuwaondolea adha wakazi wa Mkwajuni kutokana na kutokuwepo kwa Taasisi za kifedha.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuwawahutubia wananchi katika uwanja wa michezo wa Mkwajuni alivikwa uchifu na wazee wa kimila wa kabila la Kibungu wakiongezwa na Chifu Kazumba ambaye pia alimkabidhi mbuzi mnyama kama ishara ya upendo na ukaribisho wilayani humo.

Akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mkwajuni Galawa amweshukuru wakazi wa Mkwajuni kwa maaribisho mazuri na kusema kuwa changamoto zilizopo katika Mkoa wake mpya zitumikke kama fursa ya kuleta maendeleo katika wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.

Amesema Wilaya ya Songwe ina ardhi nzuri,Ziwa Rukwa na madini mbalimbali ambayo yatakuwa chachu ya maendeleo kama Dhahabu,makaa ya mawe na madini adimu duniani yanayotumika kutengezea vifaa vya elekroniki ambayo yanapatikana katika Kata ya Ngwala.

Galawa ataendelea na ziara yake katika wilaya za Mbozi Momba,Ileje na Mbozi ambapo atakuwa na kazi ya kupokea kero kutoka kwa wananchi na kuzipatia ufumbuzi ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Songwe.
 
Top