Menu
 

Na Ezekiel Kamanga,Chunya.

Zaidi ya shilingi 25.9 milioni zimeahidiwa kutolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Chunya ili kufanikisha ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti(mochwali) katika hospitali ya wilya ya chunya ili kuhakikisha changamoto hiyo inatoka hospitalini hapo.

Wadau hao wa  maendeleo katika halmshauri ya wilaya ya Chunya wametoa ahadi hizo katika kikao  na mkuu wa wilaya ya Chunya  Elias John Tarimo kujadili ujenzi wa Chumba cha kuhifadhia maiti(Mochwali) katika hospitali ya wilaya ya chunya ili kuhakikisha miili ya marehemu inasaminiwa.

Tarimo alisema ameamua kuwaita wadau wa maendeleo katika halmshauri ya wilaya ya chunya ili kuwahamasisha katika suala zima la kufanikisha  mara moja  ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya kutokana na umuhimu wake kwani ni aibu kwa wilaya kongwe kama Chunya kukosa sehemu ya kuhifadhi maiti.

Alisema lazima watambue kila mtu ni marehemu mtajiwa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuona umuhimu wa kuchangia fedha ili kuhakikisha halmashauri inapata jengo la kuhifadhia maiti.

Aidha wadau waliohudhuria kikao hicho   kwa kuona umuhimu wa jambo hilo wameweza kujitoa kwa  kupeleka mawe na mchanga lori 11,mifuko ya cement 229,na kutengeneza mirango na madirisha kwenye jengo la hilo kwaajili ya kuanza ujenzi mara moja  na kuazimia kwamba ifikapo desemba mwaka huu wawe wamekamilisha ujezi wa jengo la kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Mbali na kutoa michango mbalimbali waliweza kuunda kamati itakayokuwa ikifwatilia kwa ukaribu ujenzi wa jengo la hilo la kuhifadhia maiti hospitalini hapo ili kuhakikisha kasi hiyo inaendana na makubaliano hayo.
 
Top