Menu
 


 


Na Ezekiel Kamanga,Songwe.
 Imeelezwa kuwa zaidi ya watoto Milioni 14.8  katika bara la afrika wamepoteza mzazi mmoja au wawili kutokana na ugonjwa wa UKIMWI na Tazania ikiwemo.
Hayo yalisemwa na mratibu wa tume ya kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mbeya na Songwe Dr Edwini Mweleka katika uzinduzi wa vituo vya maarifa ya udhibiti UKIMWI vilivyopo mpemba wilayani momba na chimbuya wilayani mbozi.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara ambapo tatizo la ugonjwa wa UKIMWI  na kwamba bara la afrika ndio linaongoza kwa tatizo hilo Duniani.
Alisema hadi sasa zaidi ya watu 34 Milion duniani wanaishi na VVU ambapo zaidi ya watu mil 24 sawa na 70 wanatoka katika bara la Afrika na kusini mwa jangwa la sahara ambalo idadi ya watu wake ni 3% tu ukilinganisha na watu wote Duniani na  kiwango cha maambukizi ya UKIMWI ni zaidi ya 65% ya maambukizi yote Duniani.
Mratibu wa vituo hivyo Hadija Seja alisema kuanzishwa kwa vituo hivyo kutasaidia wananchi kupata huduma ya magonjwa mbalimbali ikiambatana na vipimo,elimu ya usalama barabarani ushauri nasaha na mambo mbalimbali yahusuyo afya yatakayotolewa bure.
Alisema lengo la kuweka mradi huo Tunduma na Mbozi  ni kutokana maeneo hayo kuwa  na mwingiliano mkubwa wa watu na maambukizi ya UKIMWI yapo juu,hivyo kuwataka wananchi kuhakikisha wanapima afya zao na kujua ili kuhakikisha wanakuwa na afya njema itakayowawezesha kufanya kazi kwa bidii.
Meneja wa mradi North Star Alliance Tom Nasongo alisema vituo vya maarifa vya kudhibiti Ukimwi hapa nchini vipo sita na vimejengwa maeneo ya Dar es salaam (2),Iringa(2) na Tunduma(2).
Alisema waliamua kujenga vituo huvyo maeneo ambayo ni maegesho ya magari makubwa kutokana na madereva hao kupata muda wa kupata elimu dhidi ya afya zao kwa ujumla,ushauri nasaha na kupata elimu dhidi ya usalama wao barabarani na kwamba hayo yote watapatiwa pasipokuwa na malipo yeyote.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Momba Richard Mbeho ambaye akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni Mstafu Chiku Gallawa aliwasihi wahudumu wa afya katika vituo hivyo kuzingatia taaluma zao na kuhakikisha wanaficha siri za wagonjwa kwani imebainika kuwa wataalam wengi wa afya huwa wanatoa siri za watu nje.
Alisema kufanya hivyo kutasababisha watu kuogopa kufika kupata huduma hapo japokuwa inatolewa bure kama wataalam hao hawatazanigatia taaluma yao,huku akiwataa wananchi kuhakikisha wanakuwa waaminifu katika ndoa zao na mahusiano kiujumla ili kfanikisha kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.
Baadhi wa madereva Saidi Mwambogolo na Sadiki Juma walisema kuanzishwa kwa vituo hivyo kutasaidia wananchi kupata huduma za afya kwa haraka hasa madereva wa masafa marefu kwani wengi wao wanakuwa hawanamuda wa kupima kutokana na kuwa barabarani muda mwingi huku wakisema wengi wa madereva wamekuwa wakiendekeza ngono jambo linalifanya maeneo ya kuegesha magari hususani mipakani kuonekana kuwa na maambukizi makubwa ya UKIMWI.
Moja wa wananchi wa  kitongoji cha Makambini(Tunduma) alisema kuanzishwa kwa vituo hivyo mpakani hapo kutasaidia kutoa elimu ya ushauri nasaha hasa kwa wananchi wanaozunguka maegesho ya magari makubwa kutokana na kuwepo kwa mwingiliano mkubwa wa madereva wa magari makubwa na wananchi maeneo hayo.

Alisema kwa kiasi kikubwa Tunduma kumekuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya magonjwa ya Ukimwi na magonjwa ya zinaa kutokana na kuwepo na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali kutokana na eneo hilo kuwa mpakani mwa Tanzania nan chi ya Zambia.

Vituo vya udhibiri wa Ukimwi  hapa nchini utaendeshwa kwa miaka mitatu na baada ya hapo wataangalia mwitikio wa watu na endapo kutakuwepo na mwitikoo mzuri wa wananchi  watahakikisha wanaendelea kutoa elimu na huduma za afya bure katika maeneo hayo na maeneo mengine hapa nchini.
 
Top