Menu
 

Kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho ameungana tena na wasaidizi wake wazamani huku msaidizi wake namba moja akiwa ni Rui Faria amekuwa Kocha msaidizi wa mashetani hao wekundu amesha fanya nae kazi katika klabu ya Uniao de Leiria ya Ureno kama kocha wa mazoezi ya viungo na akaenda naye Chelsea mara zote mbili, Inter Milan na Real Madrid.
Wasidizi 2 Ricardo Formosinho, Carlos Lalin and Emilio Alvarez have been confirmed as members of the coaching staff
Kocha Silvino Louro, ambaye amekuwa na Mourinho kwa zaidi ya muongo mmoja kama kocha wake wa makipa, pia ametajwa katika jopo la makocha wanne wasaidizi wa Mreno huyo Old Trafford.

Ricardo Formosinho na Carlos Lalin – ambao pia wana uzoefu wa kufanya kazi na Mreno huyo awali – na Emilio Alvarez pia wamethibitishwa katika benchi la Ufundi pamoja na mtathmini, Giovanni Cerra.
wasaidizi
2EAB040D00000578-0-image-a-7_1467915057099 Jose Mourinho akiwa na Faria (kushoto) na Steve Holland wakati wakifundisha Chelsea
Uthibitisho wa United wa benchi hilo la Ufundi unakuja baada ya Mourinho kujivua lawama za kuondoka kwa Ryan Giggs aliyekuwa Kocha Msaidizi namba moja.

Katika mkutano wa kumtambulisha rasmi Jumanne Old Trafford, Mourinho alisema kwamba ilikuwa ni vigumu kwa winga huyo wa zamani wa United kubaki kulingana na mazingira.
Source:- BONGO5
 
Top