Menu
 


Rapper na Hitmaker wa Mtafutaji kutoka Bongo Young Killer/Msodoki amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula baina yake na WCB."Waswahili wanakuambia vizuri siku zote havitaki haraka, kitu kizuri chochote muda wowote kinafanyika, mashabiki zangu wakae mkao wa kula baina yangu na WCB  kwa sababu wale ni wasanii na mimi ni msanii kwa hiyo kazi zinaweza kufanyika, mimi sitaki kuzungumza sana hizi mambo zikiwa tayari basi tutajuzana kwa sababu wote sisi ni wafanyabiashara naamini kila kitu kinawezekana" Msodoki ameiambia Pigia Mstari ya Kipindi cha The Splash kinachoruka kupiti Ebony FM kutoka Iringa inayosikika kupitia masafa ya 106.9 Dar es Salaam, 87.8 Iringa, 94.7 Mbeya na 88.2 Njombe.Msodoki pia amewakumbusha wasanii wenzake kuwekeza zaidi katika kutengeneza nyimbo na video zenye Ubora zaidi, ili kuendana na ushindani uliopo hivi sasa. 

''Ukifanya video kubwa unaongeza muonekano na uthamani mkubwa kama msanii na ukifanya video audio yako ikawa mbaya na video ikawa kubwa vile vile inaweza ikakupandisha au ikakushusha, na ukiwafanya audio kali na video ikawa mbaya inaweza kukupandisha aua kukushusha kwa hiyo hivyo vyote vinategemeana ili kuleta ladha nzuri ya burudani machoni na masikioni mwa watu".Pia Msodoki hivi karibuni ameachia ngoma yake ya Mtafutaji ambayo anaielezea kuwa ni ngoma yake ya kipekee ambayo ameonesha uwezo mkubwa sana katika Ku-rap na kuimba.

"Mtafutaji ndio kazi yangu ambayo kidogo kidogo ndio inayopata nafasi kwa sasa na Mashabiki ndio wanasubiri video yake kwa sasa, Video nimeshaanza kushoot nadhani baada ya wiki moja na nusu au mbili itakuwa imeshatoka" alisema Young Killer (Msodoki),


 
Top