Menu
 


Mkali wa Genge anayetamba na ngoma ya Nitulize aitwaye Brown Mauzo kutoka Nchini Kenya, amedai kumshirikisha AJE Hitmaker Alikiba katika ngoma yake kwa sababu ni msanii pekee kwa Afrika Mashariki ambaye alikuwa anafaa kuwepo katika ngoma hiyo kutokana na uwezo wake wa kuimba."Cha kwanza kabisa Alikiba ni msanii mzuri yupo katika wale miongoni mwa wasanii wazuri hapa East Afrika, Wakati tunahitaji kurekodi Song Menejimenti yenyewe ndio ili decide kwamba inaonelea vizuri Track ikiwa na sauti ya Alikiba, aaah Mimi nikaona si shwari kwa sababu gani? Alikiba akiwa ndani pale nyimbo kidogo itakuwa na Fleva tofauti, ndio tuka-decide tufanye na Alikiba, kwanza kabisa tulifanya wimbo huu ili uwe rahisi kuimbika" amesema Brown Mauzo.Brown Mauzo ambaye jina lake hilo la Kisanii limetokana na Rangi ya ngozi yake na Muonekano wake wa sura ambao huwakosha mashabiki wake mpaka kumbatiza jina hilo la Brown Mauzo."Cha Kwanza kabisa huu wimbo tumeanza kurekodi tofauti na Studio kwa Man Walter, tulianza kurekodi kwa Abby Dady lakini tulipoanza kurekodi tukasikiliza quality yake hakuwa bora kama vile mimi nilivyokuwa nataka nikaiambia Menejimenti yangu huu wimbo hujatoka kama vile mimi ninavyotaka ndio nikashauri ili itoke vizuri kama vile mimi ninavyotaka tuirejelee kwa Man Water ipigwe live na ikapigwa live ndio ikatoka vile mimi nataka" alisema Brown Mauzo.

 
Top