Menu
 

Msanii anayekuja kwa kasi katika Gemu la muziki wa Kizazi Kipya Petronia Yahya Mfaume a.k.a Petronia ameachia ngoma mpya iitwayo Nilipize.

Mwanadada huyo aliyewahi kutamba na ngoma zake kama Nikimuona, Baki nae, Nitakupendaje na ile aliyoshirikishwa na Msanii mwenzake aitwaye Chris Bee inayokwenda kwa jina la Bashee.

Petronia amesikika katika Kipengele cha PIGIA MSTARI kinachosikika kupitia Kipindi cha THE SPLASH kinachorushwa na Ebony FM Radio 106.9 Dar Es Salaam, 87.8 Iringa, 88.2 Njombe na 94.7 Mbeya na Songwe.

"Nilipize ni uandishi wake msanii Ibra Nation ambapo ndani ya hii ngoma alikuwa anazungumzia suala la kuumizwa katika mapenzi, kwa mimi nilipoisikia nilitokea kuipenda na ndipo nilipoamua kuirudia kwa maana ya kuifanyia Cover, naamini itanisogeza kwa hatua fulani" amesema Petronia.

Kwa hatua nyingine amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kumpa sapoti na namna anavyoona muziki wake unavyozidi kupiga hatua "Ugumu upo hamna kazi isiyokuwa na Changamoto, lakini sio ule ambao mimi naweza kusema kwamba nimekutana nao ikafikia hatua ya kukata tamaa ya kufanya muziki hapa"

 Download | Petronia - Nilipize Cover

 
Top