Menu
 

King of Best Melodies CHRISTIAN BELLA amefunguka kuwa hana shobo na Collabo za kimataifa.

"Kuna idea ambazo nazifanyia process, lakini bado zijaanza process yoyote kuhusu Collabo ya kimataifa, na mimi kila siku huwaga sina haraka, najua kila kitu kina wakati wake na kama nikiamua kufanya collabo nitatangaza, na sina presha pia ya collabo yoyote ya nje, nachokuwa na presha nacho nikutengeneza ngoma zinazokubalika nyumbani na maanisha Tanzania, East Africa kwa ujumla na Congo"  amesikika katika Kipengele cha PIGIA MSTARI kinachosikika kupitia Kipindi cha THE SPLASH kinachorushwa na Ebony FM Radio 106.9 Dar Es Salaam, 87.8 Iringa, 88.2 Njombe na 94.7 Mbeya na Songwe.

Kwa hatua nyingine Christian Bella amezungumzia Siri kubwa ya yeye kuwa na mashabiki wengi na ambao wanaongezeka kila siku. 

"Kikubwa msanii unatakiwa kuwa mtu wa watu, unatakiwa kuwa na despline ya kazi, pia unatakiwa kuwa mbunifu,  na mimi kinachonifanya niwe karibu na mashabiki wangu na kuongeza mashabiki wapya kila siku ni uwezo wangu wa kazi na Kikubwa Mungu anampa kila mtu nyota kwa hiyo hiyo nyota niliyopewa inamchango mkubwa wa mimi kupendwa na watu" amesema Christian Bella.

Je, kuna ujio wowote wa Malaika Band? "Ujue Amerudi nimetoa Mwaka Jana, unajua nini kitu ambacho kinawafelisha wasanii wa Bendi nikuunganisha nyimbo ambazo hazifanyi vizuri lakini unaunganisha tu, unajua kama umetoa wimbo wa Bendi inapindi uiachie time ili ufanye vizuri, wimbo kama amerudi bado una nafasi kubwa sana na bado mkubwa sana sina haraka ya kutoa wimbo na bendi labda mwaka kesho sisi hatufanyi mashindano" amesema Bella .


 
Top