Menu
 


14719776_1240319439373266_1812082732663046144_n

Hitmaker wa Ngomani, Timbulo amedai hana bifu na Vanessa Mdee aliyemchomolea kufanya naye collabo sambamba na Malaika aliyemchomolea kufanya naye video ya Ngomani iliyomgharimu muda wa kuirudia ngoma hiyo na Neylee na kisha kuifanyia video.

“Kitu kizuri niligundua tatizo liko wapi na kuli-solve. Collabo yangu mimi ilikuwa inamsaidia Malaika kuonekana kwenye video yangu ilikuwa ni msaada mkubwa sana kwake pia kwa sababu watu wangemuona na ilikuwa ni nafasi yake nyingine kuongeza step nyingine ya mashabiki, lakini pia kufanya kazi na Vanessa ilikuwa inamsaidia pia,” amesikika Timbulo katika kipengele cha Pigia Mstari kupitia kipindi cha The Splash cha Redio Ebony FM ya Iringa.

Timbulo ameongeza kuwa “Yaani kila kazi ambayo msanii unaifanya baina ya mimi inakuongea step moja ya kwenda mbele so ukiwa na hiyo imani daima huwezi kuzingua kwenye kazi ya msanii ambae unaona kabisa msanii anayefahamika na ana nafasi kubwa kwenye gemu.” 

Kwa upande Mwingine Timbulo amewataka mashabiki wake na muziki wa Bongo Flava kwa Ujumla kukaa vema kwa ujio wake mpya unaotoka mwezi huu wa Novemba.

“Tutakuwa tunasomana katika media zote naamini ni project kubwa sana ambayo pengine sijawahi kuifanya kwa sababu ya aina ya muziki ambao nimeufanya, lakini pia ni project yangu ya kwanza kufanya nje ya Tanzania nazungumzia video, so ni kitu kikubwa kila kitu kimefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu kwenye ubora wake ambao mimi sijawahi kufanya nathubutu kusema hivyo” amesema Timbulo .
 
Top