Menu
 


14714541_1226375244095442_9011835749246435328_n

Mkali wa muziki wa Genge, Nonini amefunguka kuwa ni zamu ya wasanii wakongwe nchini Kenya kurudi kwenye music industry baada ya kuwaachia wasanii wachanga nao kujitangaza ili kuongeza ushindani.

Nonini amezipigia mstari taarifa hizo wakati kupitia kipindi cha The Splash kinachorushwa kupitia Redio Ebony FM ya Iringa.

“Sisi ma-legend, maveterani turudi kwenye industry, kwa sababu hapa Kenya tumejaribu kuwaachia upcoming yaani hawa watoto wakuje, wachukue, washine, tumejaribu kunyamaza miaka kama mbili hivi, kwa sababu tuna mabiashara sisi tumekuwa wazee, tuna mafamilia nini nini… na pia miziki yetu bado ipo miziki yetu bado tuna-perfom bado miziki yetu ilikuwa imekomaa so mpaka sasa tunaperfom” amesema Nonini.

Kwa sasa muziki wa Genge/Kenya umekuwa ukihusishwa kushuka sana ukilinganisha na miaka ya hivi karibuni na kupoteza ushindani kwa Afrika mashariki na Afrika nzima Nonini amekiri pia.

“Inabidi ma-legend turudi kwa sababu ukiangalia kama sasa hivi tunarudi sote kila mtu anatoa ngoma, so natumaini the next one muziki wa Kenya utarudi mahali ilifaa kwa sababu wakongwe tunaona kweli inabidi muziki wa Kenya irudi mahali ilikuwa” amesema Nonini.

 Kwa kudhihirisha Come back hiyo ya Wakongwe tayari Nonini Mgenge True ameachia video mpya ya ngoma ya Tudunde na pia Jumatatu ijayo anaachia ngoma mpya na video mpya iliotengenezwa na Director Willy Olusu kupitia kampuni yake ya Pro Habo.
 
Top