Menu
 Siku chache tu baada ya kutangazwa kusimamiwa na Record Label ya Cheusi Dawa, mkali wa Raggae na Dancehall Big Jahman atoa somo kwa wasanii waliosainishwa kwenye label yoyote, kuachana na kasumba ya kusubiria kufanyiwa kila kitu na badala yake waweke jitihada zao binafsi.


“Kitu kikubwa ambacho watu wanatakiwa kukijua kwamba, msanii kumenejiwa au kusimamiwa na mtu, sio lazima ulipiwe video, audio, ulipiwe kila kitu unaweza pia ukajipianga ukawa na vitu vyako kama msanii mambo ya vocal na nini na nini ili kuwaacha wadau wanaokusimamia nao waendelee na kazi zao” Big Jahman amekiambia kipindi cha The Splash cha Ebony FM Redio.

Aidha, ameongeza kwa kuweka wazi mkataba wake na Record Label ya Cheusi Dawa, umejikita katika kusimamia mambo yapi? “Kwa hiyo mimi nipo chini ya Cheusi Dawa lakini kwa makubaliano yetu ambayo tumekubaliana, lakini najisimamia baadhi ya vitu vingi kama audio na vitu vingine kwa hiyo nipo deep kwenye game kwa this time.

Pakua ngoma yake mpya hapa iitwayo Mabundi akiwa amemshirikisha Fid Q na Saraha..
 
Top