Menu
 

Mkali wa Debe Tupu Tundaman, yupo tayari kukitafutia suluhisho kilio cha mashabiki wake na muziki mzuri Tanzania, ambao wamekuwa wakimdai collabo nyingine baina yake na mkali wa Aje Alikiba.


Kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka Ebony FM Radio, Tundaman ametumia kama sehemu ya kwanza, kuwapa habari njema mashabiki wa Bongo Flava nchini na kuzungumzia maandalizi anayoyafanya ili kukamilisha collabo hiyo kutokana na mashabiki kumtaka kufanya hivyo.

"Nafikiri sijawahi kuwaangusha, comment nyingi nimezipata katika ukurasa wangu wa instagram @tundamantz  kwamba ngoma ya msambinungwa umefanya vizuri sana kwa hiyo kama ungefanya kitu na alikiba so kama kuna ngoma nafikiri nafanya na ali ikiwa tayari nafikiri nitawajuza mashabiki wangu kwa ufasaha, so thanks sana kwa ngoma yangu ya depe tupu video inatoka wakati wowote" amesema Tundaman.

Tundaman afunguka sababu za video hiyo kuchelewa kutoka ambayo imefanywa na waongozaji video wawili Ivan na Hanscana.

"Nafikiri Video kuna material tu yalipotea, so nafikiri na shoot tena Alhamisi ijayo nitakuwa nimeshaimaliza kwa hiyo nitaplan lini naiachia, nafikiri imefikia hatua ya mwisho kuachia video, kuna hardish iliibiwa kwenye gari pale Posta kwenye gari ilishushwa kidogo kioo kwa hiyo watu wakaiba harddisk na laptop".

Kwa upande Mwingine Tundaman ameplan kuachia ngoma 5 mwaka huu 2017, ikiwemo aliyofanya na Yamoto Band inayosubiriwa tu video, kuna aliyofanya na Jaguar wa Kenya sambamba na ile iitwayo Mwanaume Suruali ambayo ilitakiwa kutoka baada ya Debe Tupu na akaamua kuipisha Dume Suruali ya Mwana FA.
 
Top