Menu
 Mkuki haupigwi Konzi na ukiona hasimu wako kaushika inakubidi uwe makini na mnyenyekavu kwa sababu ukijifanya mbabe utaishia kujeruhiwa na wahenga wanasema fahali wawili hawakai zizi moja.


Rapper Young Killer amekanusha uvumi uliozagaa kuwa alikuwa akimchekea Young Dee baada ya kukutana Studio kwa Producer Mona Gangster, lakini ameendelea kutamba kuwa hamuogopi Rapper huyo.

“Kila kitu kinachokuja kuhusiana na kucheka ni kwamba ni moja ya sehemu yangu ya maisha, nimezaliwa kufurahi, na furaha tumbo moja na mimi, na mimi ndio Yule mkaa kimya halafu napozwa na ulimi, amini fanikio lilipo maadui wengi  na pasipo na pesa hakuna mapenzi, kwa hiyo kama haileti hela basi hai make sense no sweat kisela au sio” amesema Young Killer.

Hitmaker huyo wa Sinaga Swagga ameongeza kuwa… “Kwa hiyo kitu kinachokuja kutokea nilivyokutana nae kwa mara ya kwanza nilikuwa katika situation ya studio, na watu walikuwemo tofauti tofauti na vingi vilivyokuwa vinanifanya nifurahi kwa sababu nilitikuwa nimeotoka kuzungumza na watu ambao niki-update vile ambavyo nimezungumza na watu mlangoni lazima nifurahi labda alihisi namchekea yeye”.

“Lakini sikumchekea yeye nimemnunia na kwenye picha nimemchana kwa hiyo ningekuwa namuogopa nadhani nisingeweza kufanya hivyo  kwa hiyo sikucheka kwa ubaya nimezaliwa kufurahi na furaha ni tumbo moja na mimi kwa hiyo iko hivyo” Young Killer amemaliza kwa kusema hivyo.
 
Top