Menu
 Mwishoni mwa juma lililopita  mkali wa midundo hapa Bongo, Luffa aliweka wazi kuwa hafanyi tena kazi na Switch Records, na sasa rasmi yupo Chini ya Wanene Studios.


Uhamisho huo unahisiwa kuwa utayumbisha kutoka kwa kazi za baadhi ya wasanii ambao walikuwa wakifanya kazi na producer huyo pale Switch Records.

Moja ya wasanii waliokuwa wa kwanza kufanya kazi na Luffa, G Nako kupitia The Splash ya Ebony FM amefungukia issue hiyo kama kutondoka kwa Luffa kunaweza kuathiri kazi zake au la?.

Yaani Sisi tunafanya kazi every where, hata ukiona picha za jana za Nick Wa Pili alikuwa anafanya kazi na Luffa, project zitatoka na tutaendelea kufanya kazi na Producer Lufa nyingi nyingi zipo na hazina tatizo lolote kutoka”.

Rapper G NAKO ameongeza kwa kutolea ufafanuzi kama kuondoka kwa Producer Luffa Switch records, naye kutamfanya kutokwenda kurekodi kazi yoyote pale.

 “Hatufanyi kazi kwa sababu mtu Fulani yupo sehemu Fulani, tunafanya kazi kutokana na uwezo wa mtu binafsi na vilevile kutokana na vibe, kama na vibe na mtu naweza kufanya kazi, kama ninakuwa sina vibe na yeye mwenyewe hana vibe hatuwezi kufanya kazi”.

Hata hivyo ameongeza kuwa kuna ngoma kama tatu zitatoka kwa mfululizo kuanzia mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao..
 
Top