Menu
 Rapper na C.E.O wa Record Label ya Cheusi Dawa Fid Q atangaza ujio wa Albamu yake ya Tatu itakayotoka mwaka huu(2017).


Taarifa hiyo ameitoa kupitia kipindi cha The Splash kinachosikika Ebony FM redio ikiwa ni siku chache tu, baada ya rapper huyo kumtangaza mkali wa Rapper na Dancehall Big Jahman kama msanii anayemsimamia kupitia record label yake ya Cheusi Dawa.

Kitu ambacho napenda ku-share na ma fans mimi kama mimi ni albamu yangu ya tatu inayotoka Kitaalogia ambayo inatoka mwaka huu Agosti 13, ikiwa na ngoma 20, kwa hiyo watu wajiandae tu mawe yanakuja zaidi” amesema Fid Q.

Pia amezungumzia uamuzi wake na record label ya Cheusi Dawa kuanza kuamua kusimamia wasanii.

“Wasio ifahamu Cheusi Dawa iliingia rasmi kwenye tasnia mwaka 2006 na ilikuwa ina-deal na masuala ya Post Production, kwa ajili ya Tv Show na kuandaa TV Shows, lakini pia cheusi dawa ilikuwa inafanya events kama contradiction lakini pia ni Record Label ambayo imemsaini Fid Q” amesema Fid Q.

Hata hivyo ameongeza kuwa “Mwaka 2017 imekuja tofauti imeanza kwa kuwasaini wasanii na kwa kuanza imeanza na Msanii Big Jahman ambaye ni msanii wa Raggae na Dancehall, nitumie fursa hii kuwashukuru watu wangu kwa kuipokea kazi yake na kuisupport”
 
Top