Menu
 Tunaamini kila mtu huwa na ndoto yake ambayo anapenda kuitimiza,lakini huwezi kuitimiza kirahisi bila kujituma na kutambua njia mbinu za kuiitimiza ndoto hiyo.


Mwanamuziki ni miongoni mwana vioo vya jamii. Tukimzungumzia Alikiba ni msanii ambaye ana mwenendo mzuri katika muziki wa kizazi kipya, ambaye anatizamwa pia na vijana ambao wanandoto yakuwa wanamuziki, ambao wamevutiwa na mazuri anayoyafanya.

Hivi karibuni ametangaza Label yake ya Kings Music ambayo itakuwa inawasimamia wasanii wenzake wa muziki akiwemo mdogo wake Abdu Kiba, Abby Skills na wengineo, na yeye moja kwa moja atakuwa kiongozi.

Lakini tukiachana na masuala ya muziki, ungependa siku moja kusikia au kuona Alikiba ni kiongozi wa nchi  au katika idara yoyote ndani ya Serikali ya Tanzania?.

“Yah kwa sababu kila mtu ana mawazo na akili ya kuchanganua na kuona hili nzuri na hili baya na maamuzi vilevile, kuwa mwanamuziki haijalishi kwamba ushindwe kufanya vitu vingine umenielewa” amesema Alikiba.

Hitmaker huyo wa Aje ameongeza kuwa “ Aaaah kwa mimi binafsi nitastick na muziki wangu, sijafikiria kabisa kuwa labda kiongozi wa nini fulani, labda nikifosiwa na wananchi kwa mapenzi yao, kwa sababu always mimi nasimama kwenye haki huo ni ukweli na dats why muziki wangu always unabase katika true stories na vitu vya ukweli ukweli”.
 
Top