Menu
 Kama utakuwa umefuatilia vizuri, utagundua ngoma kadhaa za Bonge La Nyau zilizotoka hivi karibuni hazijatengeneza na mkali wa mindundo Bongo Bob Junior ikiwemo ngoma ya Vice versa, Aza(Mtoto wa Kariakoo) na Tusiachane.


Ngoma hizo mbili kati ya hizo zimepikwa na Producer Amiga Tyger, yafaa kukumbuka kuwa Bonge La Nyau wakati akichupukia katika game ngoma kama Gusa Unase, Wengi Walaghai, Uvumilivu zilipikwa na Producer Bob Junior.

Pengine ukawa na swali nini kipo chini ya carpet, kupitia The Splash ya Redio Ebony FM, mtu mzima Bonge La Nyau ameweka wazi uhusiano wao kwa sasa.

“Ha ha ha ha haaaaaa(anacheka) hapana sifanyi kazi na Bob Junior, ha ha ha haaaaaa, eeeeh ni swahiba wangu lakini sifanyi nae kazi, ila ana kazi zake na mimi nina project zangu” amesema Bonge La Nyau.

Ameongeza pia “Hapana hapana sijakutana na athari yoyote, kwa sababu hata ukisikiliza miziki niliyokuwa nikifanya na Bob Junior kipindi hicho manyimbo ya kuchezeka chezeka, lakini sasa hivi nimeimba nyimbo za hisia, kwa hiyo nimezidi kuchukua base nimesababisha muziki wangu umekuwa na marriage kubwa naweza nikatoa wimbo ukakaa mwaka na zaidi mfano mzuri wa ngoma ya Aza (Mtoto wa kariakoo) imekaa mwaka lakini ikiipiga leo ni ngoma ambayo inaishi na itaendelea kuishi”.
 
Top