Menu
 Super Woman LADY JAYDEE aitaja rasmi tarehe 31/3/2017 kuwa ndio wakati maalumu wa kuiachia albamu yake ya Saba iitwayo WOMAN, inayotoka chini ya Record Label ya ROCKSTAR 4000.


Hitmaker huyo wa Sawa na Wao ni miongoni mwa wasanii wakongwe wenye mafanikio makubwa katika music industry katika kuutangza muziki wa Bongo Flava kimataifa, pia ni kivutio cha mabinti wengi walioingia katika tasnia ya muziki kwa kufuata nyayo zake.

Kupitia Kipindi cha The Splay ya Ebony FM Redio, amezungumzia tofauti ya Albamu ya Binti na Woman, wasanii walioshirikisha na njia atakazotumia kuiuza alamu hiyo.
BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA LADY JAYDEE


Albamu zake nyingine zilizowahi kufanya vema ni pamoja na Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), "Nothing But The Truth (2013).
 
Top