Menu
    1.      AALIYAH HOUGHTON
25/8/2001 Alikuwa akitokea visiwa vya BAHAMAS ambako alielekea kukamilisha upigaji wa picha wa video ya ngoma yake mpya…… Hivyo uhai wake ulikatishwa pale ndege waliyokuwa wakisafiria na wenzake kupata hitilafu na kuanguka muda mfupi baada ya kuruka.

Kifo cha mkali huyo wa ngoma ya I miss you ilisababisha mshituko na hudhuni mkubwa wa mashabiki wake……..

       2.      LUCKY DUBE
18/10/2007 Mkali wa Reggae ambaye makazi yake yalikuwa nchini AFRIKA KUSINI, Jina kamili ERMELO PHILIP DUBE aliuawa kwa kupigwa risasi nje kidogo ya jiji la Johannesburg, muda mfupi baada ya kuwapeleka wanae shule.

Jamaa alikuwa ndani ya gari aina ya CHRYSIER 300C alipozingirwa na wanaume wenye silaha ambao walimfyatulia risasi zilizohitimisha uhai wake.

       3.      PETER TOSH.
  11/9/1987 aliuawa kwa kupigwa risasi jirani na nyumba yake Nchini JAMAICA chanzo cha kifa chake kinadaiwa kutokana na kujiunga na Mambo ya kisiasa.

Alikuwa mwanaharakati wa Mrengo wa Kushoto na ni miongoni mwa waasisi wa   THE WAILERS iliyokuwa chini ya Nguli wa Reggae BOB MARLEY.

     4.      NOTORIOUS B.I.G
19/3/1997  Jina kamili ni CHRISTOPHER WALLACE Gangstar Rapper ambaye alikuwa kivutio cha mashabiki duniani kote na alikuwa katika kundi la Wana Hiphop wa EAST COAST, Katika Jiji la NEW YORK MAREKANI jinari na makazi yake ndiko alipopigwa risasi.

      5.      JOHN LENNON.
8/12/1980 aliuawa kwa kupigwa risasi nne mgongoni na MARK CHAPMAN nje ya nyumba yake jijini NEW YORK, MAREKANI…….. Jamaa LENNON alikuwa muimbaji wa kundi la THE BEATLES.

  Sababu za kutwangwa risasi kwa mkali huyo hazijafahamika mpaka sasa na  Mamilioni ya watu walijitokeza kuomboleza, akiwepo mke wake YOKO ONO.

       6.      MARVIN GAYE
1/4/1984 Siku moja tu kabla ya kuadhimisha, kutimiza umri wa miaka 45, alipigwa risasi na Baba yake mzazi huko LOS ANGELES nchini MAREKANI kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia unaodaiwa kuwa GAYE alikuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja……(maarufu kama SHOGA) na matumizi ya madawa ya kulevya ukiwemo Unga.

Hali hiyo ndiyo iliyopelekea Baba yake kuona kama akidharirishwa na kuamua kumpiga risasi…….

       7.       KURT COBAIN
5/4/1994 Kiongozi wa kundi maarufu la Pop Alipigwa risasi wakati akijaribu kutoroka Gerezani huko LOS ANGELES nchini MAREKANI.

Mashabiki wengi wa kundi hilo nao walijipiga risasi na kufa mara baada ya kupata taarifa za kifo cha KURT, ikiwa ni njia ya kupinga ukatili wa askari magereza kwa watu wanaoshikiliwa gerezani.

      8.      TUPAC AMARU SHAKUR
1994 jaribio la kwanza lilifanywa ambapo alipigwa risasi lakini akanusurika kifo.

13/9/1996 Likawa ni jaribio la pili kwa Gangstar Rapper huyo aliyeacha historia ya ngoma kibao kama DEAR MAMA alipigwa risasi nne wakati akitoka kutizama mpambano wa ndondi kati ya Swaiba wake wa karibu MIKE TYSON dhidi ya BRUCE SELDON huko LAS VEGAS.

 9.  LISA LOPES “LEFT EYE”
25/4/2002 alipatwa ajali ya Gari aina ya Mitsubishi Pajero alilokuwa akiliendesha mwanadafada huyo wa kundi la TLC akiwa na abiria watatu wakati akijaribu kulipita Roli kubwa lililokuwepo mbele yake alipokuwa aki-overtake, akaona gari lingine likija kwa kasi mbele na kufanya jitihada za kuepuka kugongana uso kwa uso.

Jitihada zake akalielekeza gari lake pembeni ya barabara na kugonga miti na kubiringika mara kadhaa na kumsababishia mauti yake .

Mrembo huyo anaendelea kukumbukwa kutokana na mvuto wa kipekee, hali iliyopelekea kuwatia majozi mashabiki wake kutokana na Majeraha makubwa aliyopatwa  kichwani na shingoni.

     10. MOSNTANE TALBERT “M-BONE”
16/6/2011 Rapper huyu kutoka kundi la CALI SWAG DISTRICT ya nchini MAREKANI aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake kitaa.. cha CALIFORNIA.

Jamaa aliuawa siku kadhaa baada ya kuachia ngoma yao kama kundi inayokwenda kwa jina la “TEACH ME HOW TO DOUGIE” kuanza kupata utambulisho wa kimataifa.
 
Top