Menu
 Waziri mkuu amewataka viongozi kutowatangaza watuhumiwa wa dawa za kulevya bila ya kufanya uchunguzi lakini wasiogope kuwaanika wale wenye uhakika kuwa kweli ni wauzaji.

Ameyasema hayo wakati akizindua Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya katika ofisi ya Waziri Mkuu Ijumaa hii. Alisema wakuu wa mikoa wana nafasi nzuri ya kushiriki katika vita hiyo kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu. 

Alisema, “Kuendelea na zoezi hili Watanzania wanataka kujua hii vita inaendaje, msisite baada kuwakamata, mmejiridhisha kuwatangaza hadharani iwe mfano kwa wengine wote ambao wanakusudia au wanaendelea kwa siri kutumia au kujihusisha kwenye jambo hili la uchunguzi ambao utakuwa unaendelea. 

Watendaji wa mamlaka kila mmoja kwa nafasi yake mnapaswa kufahamu kuwa mmeaminiwa hivo inabidi muwe waadilifu sana kwani mmekabidhiwa majukumu makubwa yanayohitaji uangalifu wa hali ya juu.”

Aidha waziri mkuu alisema serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria kiongozi yeyote atakayejihusisha na rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

By: Emmy Mwaipopo
 
Top