Menu
 Mwanamke mzito zaidi duniani, akiwa na uzani wa kilo 500, amefikishwa nchini India atakapofanyiwa upasuaji wa kumsaidia kupunguza uzani.
 
Eman Ahmed Abd El Aty, mwenye umri wa miaka 36 alifika mjini Mumbai jana (Jumamosi) kutoka mji wa Alexandria nchini Misri. 

Ripoti kutoka kwa jamaa zake zimedokeza kwamba Abd El Aty hajatoka nyumbani mwake kwa zaidi ya miaka 25 kwa sababu ya kushindwa kudhibiti uzani wake. 

Abd El Aty alinyimwa visa na ubalozi wa India mwaka uliopita kwa sababu hangeweza kufika katika ubalozi huo. 

Hatimaye alipata visa baada ya daktari wake kuzungumzia hali yake kwa waziri wa mambo ya nje.
 
Top