Menu
 Hitmaker wa One Day aitwae Nandy, amesema wasanii wakike wengi hukata tamaa katika muziki kutokana na kupenda kufanyiwa kila kitu na ndio maana unaweza kukutana na wimbi kubwa la wasanii wakike wenye vipaji ambao wameachana na sanaa.Nandy amekiambia kipindi cha The Splash kinachosikika kupitia Ebony FM chini ya Watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji na ku-share nao mbinu za kuzingatia kwa wasanii wakike ili kujinasua katika vikwazo na hatimaye kufanikiwa ambazo pia yeye binafsi alizizingatia.

“Cha kwanza mwanamke kama mwanamke hatakiwi kukata tamaa, aaah kila mtu ana vitu vyake anavyopitia, yeye mwenyewe anajua kwenye moyo wake, lakini kilicho kikubwa sisi wanawake tumeumbwa ku-fight, hatujaumbwa kukata tama, huu muziki upo tu naamini kila mtu kaandikiwa muda wake, kama mimi watu wengi wanavyojua sijaanza juzi tu kuimba lakini Mungu labda kaniandikia kuanzia mwaka jana, mwaka huu na kuendelea hatuwezi jua”.amesikika Nandy.

Nandy ameongeza kwa kutoa ushauri “Kikubwa wasikate tamaa wamuweke Mungu Mbele wasali sana, wafanye kazi kwa bidii, sisi wanawake tunapenda short cut kufanyiwa kila kitu tofauti na wasanii wakiume, wasanii wakiume tukiongelea Hustling kweli wana hustle tuvae uhusika kama wasanii wakiume vaa uhusika wa maisha yako kwa sababu muziki una hela sitanii muziki unaboresha maisha wafanye miziki kadhaa watafute Connection”

 Pia ametaja muda wa kutoka kwa video yake ya One Day, “Video ya One Day probably this week inaweza kuwa tayari nimeshoota hapahapa Tanzania, lakini kwa upande wa Director naomba iwe surprise kwa ma fans wangu na wananchi kwa Ujumla”
 
Top