Menu
 

 


Msanii wa muziki Q Chief amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya mambo mazuri ingawa kwasasa hayupo chini ya label yoyote.

Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni aliachana na label ya QS Mhonda, ameiambia Bongo5 kuwa kuachana na label hiyo siyo mwisho wa maisha yake kwani kuna mambo makubwa yanakuja.

“Mimi naamini binadamu tunapanga yetu na Mungu anapanga yake, kwahiyo kilichotokea ni sehemu ya maisha ya binadamu, QS Mhonda hajaondoka na kipaji changu bado nafasi ninayo ya kufanya mambo makubwa zaidi, kikubwa ni kumtanguliza Mungu mbele,” alisema Q Chief.

Aliongeza, “Pia namshukuru kwa yote aliyonifanyia, amenitoa sehemu moja na kunipeleka sehemu nyingine na sasa mimi binafsi naanza kupambana ili kuangalia nampeleka Q Chief katika hatua nyingine, ikitokea label ambayo itanihitaji kwajili ya kazi tutafanya, lakini mpaka sasa hakuna label ambayo imejitokeza lakini kuna baadhi ya watu niko nao kwenye mazungumzo,”

Muimbaji huyo aliachana na label yake ya zamani baada ya kushindwana kuwekana sawa kwenye masuala la mkataba.
 
Top