Menu
 

Uongozi wa kampuni ya QS Mhonda inayomsimamia muimbaji mkongwe, Abubakar Katwila aka Q Chillah, umesema hadi sasa umeshatumia takribani shilingi milioni 200 kwaajili ya msanii huyo na haujawahi kupata faida.


Meneja Obama anayewasimamia wasanii wa bosi QS Mhonda, amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa wametumia kiasi hicho kwa kipindi cha miezi 29 tangu walipoanza kuwa naye lakini kwa mwaka wamekuwa hawaingizi hata milioni tano kutoka kwa msanii huyo.

Meneja huyo ameongeza kuwa fedha hizo ambazo uongozi huo umezitumia kwa Q Chillah ni pamoja na kulipia video ya ‘Sungura’ ambayo imewagharimu milioni 37, kumlipa Patoranking milioni 25 kwa ajili ya kolabo ya wimbo wa ‘Koku’ na matumizi mengine binafsi. 

Kwa upande wake Q Chillah amedai kuwa kwa sasa ana jambo moja la mwisho ambalo anataka kufanya kwa bosi wake huyo. Q-Chillah amesema tayari ameshamtumia Mhonda barua mbili lakini kwa sasa anatarajia kumtumia barua ya tatu na yabmwisho kwa ajili ya kumshukuru na kuthamini mchango wake kwa kule ambapo amemtoa.

“Tayari nimeshatuma barua mbili kwa QS, sasa nataka kutuma barua ya mwisho ambayo itakuwa ya tatu kwa ajili ya kumueleza natambua mchango wake kutokana na kule aliponitoa,” amekiambia kipindi hicho.

Hivi karibuni ndugu wa msanii huyo walilalamika kuwa tangu Chillah aanze kusimamiwa na kampuni hiyo, hawaoni lolote la maana alilonalo na maisha yake yameendelea kuwa ya kubangaiza.

 
Top