Menu
 

Ilikuwa pigo kubwa sana kwa wapenzi wa mziki wa RAP na HIPHOP mwaka 1996 baada ya kumpoteza mmoja wa muimbaji maarufu wa mziki huu duniani, TUPAC, AMIR SHAKUR “HIPHOP ICON”. 

Sababu ya kifo chake kimehusisha na mambo mengi sana lakini mpaka hii leo ukweli halisi haujaweza kujulikana ya kwamba ni nani aliyehusika na njama za mauaji ya marehemu TUPAC.

Alikuwa Rapa mwenye vibweka vingi na hakuna aliyeweza kufananishwa nae. Ukorofi wake akiwa stejini na hata mtaani hakuna aliyeweza mgusa kwani alikuwa tayari kwa kila kitu.

Tupac amekulia kwenye mazingira ambayo kama mtu angepata kushuhudia hali halisi ya maisha ya rapa huyu basi asingebisha kama angeambiwa kuwa ni mhalifu mkubwa huko mjini NEWYORK. 

Mama mzazi wa marehemu Tupac, ALICE FAYE WILLIAMS na baabae kujibadilisha na kujiita AFEN SHAKUR, aliacha shule na kuamua kujiunga na kundi moja la wahuni lililojulikana kama Carolina Gangs, na baadae kuachana malo baada ya kuona halina manufa kwake na kuhamia Brooklyn..

Huko alikuwa mmoja ya watu weusi ndani ya chama kilichoitwa “Black panther” ambacho kilikuwa na maudhui makubwa ya kuondoa unyanyasaji wa watu weusi nchini Marekani. Akiwa ndani ya chama hicho, alianzisha mahisiano ya kimapenzi na mmoja ya walinzi wa Malcom x na akawa mwanasiasa rasmi.

Mwanamke shupavu aliyejitolea mhanga kupigana mpaka haki ipatikane baina ya watu weusi nchini Marekani. Afeni aliachana na mlinzi wa Malcoln x na kuanzisha mahusiano mapya ya kimapenzi na mmoja kati ya waandaaji wa chama hicho, Aliyejulikana kwa jina la Lummumba.

Hapo walifanya mambo mengi yakiwa ni pamoja na kuung’oa utawala wa kizungu uliokuwa wa unyanyasaji nhini humo. Wakiwa kwenye njama hizo Afeni alikamatwa baada ya siri hiyo kubainika na kutupwa jela pamoja na wenzake ishirini.

AFEN aligundua kuwa anamimba ya Lumumba lakini bwana huyo alikataa na kusema hahusiki kabisa na ujauzito huo na hapo akiwa gerezani alikataliwa na Lumumba. 

Akiwa kwenye gereza la wanawake huko Greenwich aliweza kulilia haki yake mpaka kutolewa gerezani akiwa mjamzito na hapo aliapa jina la motto atamwita “Prince” kwa vyovyote vile na atataka mtoto huyo kuwakomboa watu weusii wanaobaguliwa.

Ulikuwa ni mwaka 1971, tarehe 16 mwezi wa 6 ambapo AFEN SHAKUR alisikia uchungu na kujifungua salama mtoto wa kwanza na kumuita jina la Lesssane Parish Croons na baadae kumuita Tupac Shakur akiwa hana baba. 

Huo ndio mwanzo wa aliyewahi kuwa rapa maarufu duniani, Marehemu Tupac Shakur. Mama mzazi wa Tupac alimlea mtoto wake huyo katika mazingira ya tabu sana. Enzi za Tupac, watu waliomfahamu kwa kumuita “Black Prince”kwa kuwa mama yake alimpenda mtoto wake.

Marehemu TUPAC alikulia katika mazingira ya kitemi kwa kuwa hakuweza kupata malezi bora ya wazazi kwa kuw mama yake hakuwa na muda wa kukaa nhini na kulea mtoto ingawa alimpenda sana. 

Alikuwa anamsumbua sana mama yake kuhusu kumjua baba yake na mama huyo hakuwa na jibu la kuweza kumridhisha zaidi ya kumwambia ipo siku atakuja.

Akiwa na miaka miwili tu, TUPAC alipata mdogo wake wa kike aitwaye Sekyiwa, naye hakupata kumuona baba yake kwa kuwa alikamatwa kwa wizi wa gari na kuhukumiwa kifungo cha miaka sitini jela hivyo Afeni aliwalea watoto wake chini ya uangalizi wake mwenyewe. 

Waliishi maisha ya tabu sana na waliamua kuhamia sehemu nyingine iitwayo Bronx na huko familia ilitawanyika ingawa walikuwa wadogo lakini iliwalazimu waende kutafuta hela ili waweze kuishi lakini mwisho wa siku wanakutana nyumbani nakugawana kile walichopata.

TUPAC hakuwa na marafiki waliokuwa wanamkubali kama mmoja ya wanajamii kwa kuwa waliamini mtoto huyo ni ambao ni wahuni hivyo hakuwa na marafiki zaidi ya kuishi maisha ya peke yake. Aliishi maisha ya tabu sana huku akiwa anateseka juu ya suala la kutomjua baba yake. 

Kuanzia kipindi hicho, Tupac alianza kuandila mistari ya mapenzi ili kuweza kuwafariji kwa kuwa alikuwa mpweke kiasi cha hata ndugu zake kwa upande wa mama hawakuweza kumkubali.

TUPAC alikuwa na kitabu kikubwa kama kitabu cha kutunzia kumbukumbu muhimu na ndani yake aliandika ya kwamba siku mmoja atakuja kuwa mti maarufu sana duniani. 

Alipenda sana kuigiza na aliona huko ndipo umaarufu wake utakapojengeka vema na aliona ya kwamba anaweza sana kuigiza.

Mtoto anapewa kile anachotaka hivyo ilikuwa kwa mama wa TUPAC, AFENI aliamua kumpeleka mtoto wake wa pekee wa kiume kwenye kituo maalumu kilichokuwa kinajihusisha na masuala ya sanaa huko Manhattan. 

Huko aliweza kufahamika akiwa na umri wake mdogo kutokana na kuweza kupatia kwenye suala la uigizaji na hapo aliona ya kwamba ndugu zake wataweza kumheshimu kutokana na watu baki kuanza kumkubali katika jamii.

Akiwa huko, TUPAC alianza kuupenda muziki wa rap na hapo aliachana na mistari ya mapenzi na kuangikia kwenye rap. 

Aliweza kufahamika kwa jina la “Mc New York” ndani ya New York kwa ajili ya kuweza kumudu kurap na watu walifikiri ya kwamba alikuwa mtu mmoja mkubwa sana lakini pale alipotokeza mbele ya watu na kujitambulisha kama Mc New York kila mtu alishangaa.

Alijiunga na shule moja iitwayo “Baltimore school for the arts” ambapo alikutana na watoto wenye rangi nyeupe ambao alitokea kuwachukia sana lakini baadae aliweza kuishi nao vizuri kwa kuwa aliamini kuwa watu weupe wote ni mashetani.

 Kuanzia hapo TUPAC aliona ya kwamba yeye ni msanii ambaye anauwezo wa kufanya chochote anachotaka baada ya kupata mafunzo aliyoyapata shuleni hapo.

Akiwa na miaka ishirini tu, TUPAC alikuwa tayari ameshakamatwa mara nane na kuwekwa kituo cha polisi mara tano akiwa anashikiliwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuwa na kikundi cha uhalifu, kuiba, ukabaji na kuhusishwa na kifo cha mtoto wa miaka saba.

Baada ya hapo aliungana na marapa wengine ambao kwa kipindi hicho walikuwa hawafahamiki kama HUMPTY-Hump a.k.a Eddie Humphrey, “SHOCK G” na kuunda kikundi cha kurap ambapo mwaka 1990 walifanikiwa kutoka na albam iliyoitwa “sex packets” na baada ya hapo kusambaratika.

Mwaka 1992, TUPAC aliamua kutoka na albam yake ya kwanza iliyoitwa “2PAC ALYPSE NOW” ambayo ilimuweka kwenye ramani ya waimbaji bora wa HIPHOP nchini Marekani , kwa kuwa aliweza kukubalika na kupata mafanikio. 

Mwaka huo huo aliweza kucheza filamu iliyoitwa “JUICE”, ambayo ilikuwa inahusu maisha ya halisi kihuni nchini Marekani, ambayo iliweza kuuzwa duniani kote na kumpa mafanikio makubwa.

Mwaka 1993, TUPAC aliachia albam yake ya pili iliyoitwa “STRICTLY 4 MY NIGGAZ” ambayo iliweza kuuzwa na utajiri ulimtembelea rapa huyo. Kipindi hiki kilikuwa cha neema kwa familia maskini ya rapa huyu kwani aliweza kulekebisha toka kwenye maisha waliokuwa wanaishi ya kimasikini na kuwa na hali nzuli.

 Mwaka huo huo TUPAC na Janet Jackson walicheza kwenye filamu iliyoitwa “POETIC JUSTICE” ambayo iliweza kuuza nakala zaidi ya milioni tatu jinsi watu walivyoipokea filamu hiyo.

Mwaka 1994, TUPAC alipigwa risasi tano na kufanikiwa kuokoka kwenye kifo baada ya wezi kumvamia na kuiba vito vyake vya thamani vya dola za kimarekani elf arobaini.

Mwaka 1995 aliachia albam yake iliyoitwa “ME AGAINST MY WORLD” ambayo alifanikiwa kuuza nakala milioni mbili. Hakuweza kukaa sana baada ya kuitangaza albam hiyo, Mwaka 1996 aliachia albam nyingine “ALL EYES ON ME” ambayo aliuza zaidi ya albamu yake iliyopita.

Hiki ndicho kipindi ambacho TUPAC alikuwa ameanza kupata mafanikio makubwa na ndipo nyota yake ilizimika ghafla baada ya watu wasijulikana kumpiga risasi baada ya kutoka kuangalia pambano la Mike Tyson akiwa ndani ya gari la mshirika mwenzake KNIGHT ilikuwa tarehe saba mwezi wa tisa na kufariki tarehe kumi na tatu mwezi huo huo baada ya jitihada za madaktari kushindikana..

Kifo cha rapa huyo maarufu duniani ilikuwa pigo kubwa sana kwa wapenzi wa mziki wa Rap duniani. Ingawa na yote haya TUPAC aliwahi kusikika akisema hataweza kufikisha miaka thelathini kwani atakuwa si hai kutokana na kuotea kifo chake mara kwa mara na kitakuwa ni cha ghafla sana pamoja na kuwasikitisha wapenzi wake wote duniani.

Jina Makaveli lilikuja baada ya kupigwa risasi mara tano mfululizo na watu wote kufikili amekufa na baadae kupona kifo hicho. Makaveli alikuwa mtu mmoja hapo zamani aliyesadikika kufa kwa kupigwa risasi na baadae kuonekana sehemu nyingine akiwa hai..

Baada ya kifo chake lebo ya marehemu TUPAC imesha toa albamu zipatazo kumi na nne zikiwemo “The Don Killumati”, Pacs Life”, “Ready to die” Loyal to The Game” na nyinginezo chini ya jina Makaveli.

Marehemu TUPAC ameacha pengo kubwa sana kwenye mziki wa Rap na daima atakumbukwa kwa yale yote aliyofanya kuinua mziki wa rap uweze kukubalika duniani kote na kutokuonekana wa kihuni pamoja na uzalendo wa kuipenda rangi yake nyeusi.

Mpaka kifo chake alikuwa karibu sana na wenzake kama “Dr Dre”, “Suge”, “Knight”, ambaye alikuwa raisi wa rekodi ya “DEATH ROW”, “ Snoop Dog”, “Mike Tyson”, rapa “Mc Hammer” ambaye walikulia sehemu moja walipokuwa wadogo.. Tupac alikuwa anataka kumuoa mwanadada “JONES”..

Alikuwa adui mkubwa wa marehemu “NATORIOUS BIG” alikufa mwaka uliofuata kwa kupigwa risasi. Uadui huo ulikuwa hasa juu ya Tupac kutangaza rasmi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa BIG pamoja na kutoa wimbo ambao ulikuwa unamkejeli BIG.
 
Top