Menu
 Kama ulikuwa na shauku kubwa yakuosikia siku moja collabo baina ya hitmaker wa Mazoea Billnas na Godzillah hujakosea kwani kama ikitokea nafasi ya kufanya inawezekana ukaisikia.


Mara kadhaa kumekuwa na stori za hapa na pale kuwa rapper Billnas amekuwa akimgeza sauti ya kurap rapper Godzillah, hali ambayo imekuwa ikipingwa vikali na Billnas.

"Kufanana sauti ni watu wameamua kusema hivyo, kwa sababu sikiliza nyimbo zangu, sikiliza nyimbo zake, sikiliza pata nafasi ya kuchambua vizuri unaweza kuiona tofauti" amesikika Billnas kupitia kipindi cha "The Splash" kinachoruka Ebony FM redio.
 
Billnas amezungumzia wazi mipango ya collabo yake na Godzillah, "Aaaaah inshallaaaah, ikitokea panapo majaliwa tunaweza kufanya nae wimbo, mimi nafikiria kuwashirikisha wasanii wengi kadri muda unavyoenda na pia nahitaji kusikika mwenyewe sana sana kwa namna moja ama nyingine".
 
Top