Menu
 

Mwezi Februari, 2017 ulikuwa wakati sahihi uliotangazwa na Mfalme wa RnB Tanzania Bernad Paulo a.k.a Ben Pol kuwa angeachia albamu yake ya pili iitwayo Ben Pol.


Kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka redio Ebony FM, hitmaker huyo wa Phone amesikika akiwajibu watangazaji wa kipindi hicho Chris Bee na Fredoo Mbunji, sababu zilizochingia kwa albamu hiyo kushindwa kutoka kwa wakati muafaka.

"EP yangu au albamu yangu ya Ben Pol, ni kweli nilipanga niitoe mwezi wa pili lakini bado tupo kwenye mazungumzo na watu waku-distribute" amesema Ben Pol.

Aidha ameongeza kuwa "Kwa sababu unajua huwezi kutoa albamu, kama hakuna mifumo mizuri ya kuipitisha ile albamu kuwafikia watu kwa hiyo hicho ndio kitu sasa hivi tunaendelea nacho majadiliano, yakuweza kuhakikisha tunapata distributors, kampuni nzuri wadau wazuri wa kuwezesha albamu kuwafikia watu wengi".

 
Top