Menu
 Washindi wa Tuzo ya Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya kwenye Kili Music Awards mwaka 2013, Jambo Squad usiku wa leo Ijumaa ya Machi 3 wanatarajia kuachia video yao mpya ya Mamiloo.


Kundi hilo lenye masikani yake Jijini Arusha, limerudi kwa kishindo kwenye Music Industry na ngoma hiyo baada ya ukimya wa miaka mitatu uliosababishwa na kupatwa ajali sambamba na crew member mmoja wapo Nigga C a.k.a Chalii Jambo kufiwa na Mama ake mzazi.

“Video ikifika mida ya Saa 3, saa 4 au saa 5 usiku tutakuwa tayari tumeshaiweka kwenye mtandao kila mtu ataiona”. Nigga C a.k.a Chalii Jambo amesikika na Exclusive hiyo kupitia kipindi cha The Splash kinachosikika kupitia redio Ebony FM kinachoongozwa na Chris Bee na Fredoo Mbunji.

“Hii video tumefanya na chalii mmoja hivi mbaya sana anaitwa Director H, anaitwa Humprey lakini jina mbalo watu wengi wanamjua anajulikana kama Director H” ameongeza Nigga C a.k.a Chalii.

 
Top