Menu
 Baada ya ukimya wa miaka mitatu Kundi la muziki wa kizazi kipya lenye Maskani yake Jijini Arusha Jambo Squad wametu-bless na ngoma ya Mamiloo iliyotoka siku ya Jumatatu Februari 27, 2017.


Pengine ukawa ulikuwa unajiuliza maana halisi ya Mamiloo ni nini kama mimi lakini jibu halisi tumepata kutoka kwa crew member wa Jambo Squad aitwae Nigga C a.k.a Chalii Jambo.

“Mamiloo ni kama unavyosema baby, kama unavyosema darling, kama unavyosema mpenzi sasa huku Arusha hawatumii sana baby, wanatumia Mamiloo au Mamalai tulihitaji tufanye ngoma fulani ya mapenzi tumuimbie baby fulani ambaye ni Wife material Fulani unataka kumuoa ndio tuka decide iitwe Mamiloo” amesema Nigga C kupitia The Splash ya redio Ebony FM.

Kwa hatua nyingine amezungumzia ukimya wao. “Ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria, kwa hiyotulikuwa tunaandaa vitu vizuri tulikuwa tunajipanga tuje na mashambulizi mazuri ndio maana ukisikiliza hii ngoma ni chafu sana yaani tumepiga stayle Fulani ambazo kila mtu hakutegemea”.

BOFYA HAPA CHINI KUSIKILIZA MAMILOO – JAMBO SQUAD
 
Top