Menu
 Mwanamuziki mkongwe na mwenye heshima kubwa katika muziki wa Bongo Flava na Hitmaker wa “Sawa na Wao” Lady Jaydee, ametupa tofauti ya albamu yake ya pili iitwayo Binti iliyotoka mwaka 2003 na albamu yake mpya ya Woman inayotoka Machi 31, mwaka 2017.


“Albamu hii ya Woman na Binti zinatofauti, kama albamu nyingine zilivyotofauti, Binti ilikuwa ni albamu ambayo ni binti ambaye amepitia mambo kuumizwa kimahusiano na kuumizwa kimaisha lakini akapata nguvu akasimama, kwa hiyo albamu ya binti ilikuwa ni albamu ya kumpa nguvu binti aweze kunyanyuka kutokana nay ale aliyoyapitai na aweze kusonga mbele na maisha” Lady Jaydee amekiambia kipindi cha The Splash cha redio Ebony FM.

“Lakini albamu ya Woman ni mwanamke ambaye tayari ameshakua, ameshapitia vitu vingi, anaijua furaha yake, anajua sehemu yake ya kusimama katika maisha, kwa hiyo nyimbo za humu si nyimbo za masikitiko sana na si nyimbo za furaha sana tu yaani sio kitu tu kimoja cha kuelezea mlengo wa humu ukoje, lakini na mwanamke ambaye amepitia vitu vingi na anawakilisha vitu vingi ambavyo wanawake wengine wameweza kuvipitia katika maisha yao”ameongeza Lady Jaydee.

 Albamu zake nyingine zilizowahi kufanya vema ni pamoja na Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), "Nothing But The Truth (2013).
 
Top