Menu
 Female Rapper Chemical, anatarajia kuachia Filamu yake mpya iliyopewa jina la "Mary Mary" aliyofanya na msanii mkongwe wa filamu nchini na aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2016 Wema Sepetu.


“Kuna movie nime-shoot na Wema Sepetu, watu wengi wanasema itatoka lini, itatoka lakini nasubiri muda ambao nitakuwa free zaidi” Chemical amesikika amesikika katika kipindi cha The Splash kinachosikika kupitia redio Ebony FM kinachoongozwa na Chris Bee na Fredoo Mbunji.

“Kwa sababu nahitaji advertisement tunahitaji promotion, I have to be free na vito kama shule, yah kwa hiyo nikiwa na muda mwingi ndio itatoka pale kwa sababu namaliza shule mwaka huu wa 2017 nafikiri mwezi wa 7” ameongeza Chemical.

Hata hivyo filamu hiyo ilitakiwa kutoka mwezi Disemba mwaka 2016 na walianza kui-shoot mwezi Novemba na ikielezea adha wanayokabiliwa nayo watoto wa mitaani.  

MSIKILIZE HAPA CHINI.
 
Top