Menu
 Baada ya kupokelewa vema na kujivunia mafanikio ya ngoma ya Matobo iliyoimbwa na kundi jipya la muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania Madada Sita, Uongozi wa Mkubwa na Wanae unaolisimamia kundi hilo umepanga kutoa zawadi kwa kila mdau wa muziki, media na mashabiki.


Ebony FM Redio kupitia kipindi chake cha burudani cha The Splash kilikuwa na Exclusive hiyo kutoka kwa Meneja wa kundi hilo Chambuso na kiongozi wa kundi hilo Emmy Wimbo walifungukia aina ya zawadi waliyopanga kutoa.

“Baada ya Matobo, Jumatatu ya Machi 13, 2017 tunategemea kutoa wimbo mpya pamoja na audio nadhani kesho tutakuwa tunafanya video yake kwa kumalizia baadhi ya vipande, wimbo tumefanya kwa producer anaitwa Mesen Selekta na video tunafanya na Director anaiwa Tonee amesema Meneja Chambuso.

Akizungumzia maudhui ya wimbo huo Meneja Chambuso amesema “Tumerudi kwenye jamii kidogo tumeongelea watu wenye midomo midomo, wanaosema mara hiki hakiwezi kuwa hivi yaani wanakushusha, hawajui kama Mungu atakupa nini sasa umekuja kupata sasa na wewe unaanza kujigamba yaani tunaongelea majibuno kama watu hawakutegemea utakuja kupata kitu Fulani au umefanikiwa kuwa mtu Fulani sasa umepata unamuambia wewe sio Mungu, Mungu amenipa”.

Kwa upande wake Emmy Wimbo kiongozi wa kundi hilo amezungumzia mwenendo na ushindani wao kama kundi la Madada Sita katika gemu la muzki wa kizazi kipya.

“Gemu ipo vizuri   na tumeona wimbo wetu wa kwanza umepokelewa vizuri na fasta tu tayari tumeona tutoe wimbo mwingine, kwa sababu tumeshaona mashabiki wanaanza kuelewa taratibu taratibu hivyo hivyo tutafika lakini mwanzo mzuri”.
 
Top