Menu
 Label ya Mkubwa na Wanae na Tanzania Bora Initiative wakutana katika kikao cha pamoja na kumjadili msichana na mwanamke au wanawake wenye vipaji katika kujiletea maendeleo.


Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanae Said Fella a.k.a Mkubwa Fella amefunguka zaidi agenda zilizolengwa katika kikao hicho kilichowakutanisha pamoja na wasanii waliopo katika label hiyo.

“Kwanza wasichana kujitambua na vilevile kuchukulia kwamba wanaweza kujisaidia(kujipatia kipato na mafanikio) kupitia vipaji vyao, kwenye elimu na sio kupitia miili yao” amesikika Said Fella kupitia The Splash ya Redio Ebony FM inayosikika kupiia masafa haya 106.9 Dar es Salaam, 94.5 Mbeya, 87.8 Iringa, 88.2 Njombe na Songwe 94.5.

Ameongeza “Kuna hawa wenzetu wanaitwa Tanzania Bora tumfungana mkataba, tunawasaidia nini Wadada hususani kwa kupitia haswa hawa Madada 6 kwamba wanatumia vipaji vyao ili mradi waje wajikomboe na maisha yao”.

Kwa upande mwingine Mkubwa Fella anaendelea kutueleza agenda namba mbili iliyojadiliwa kupitia kikao hicho, “Kingine kuangalia Bongo Flava ilipo na inapotaka kuelekea”.

Hata hivyo Kundi la Madada 6 wameachia ngoma yao ya pili iitwayo Bakari imeandikwa na Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanae SAID FELLA a.k.a Mkubwa Fella na wasanii wawili kutoka Yamoto Band Beka Flava na Aslay chini ya utayarishaji wa Producer Shirko.
 
Top