Menu
 Kwa sasa wasanii kote duniani  wamekuwa wakichuana kwa kufanya ziara za kimuziki katika maeneo mbalimbali huku wengine wakivuka mipaka zaidi. 


Kundi bora Afrika Mashariki na Afrika Navy Kenzo linaloundwa na wakali hawa Nahreel na Aika limetangaza rasmi kuanza ziara yake iliyopewa jina la “AIM World Tour”.

Nahreel amesikika na exclusive hiyo kwenye kipindi cha The Splash ya Redio Ebony FM kinachotangazwa na Chris Bee na Fredoo Mbuji.

“Tumeipa jina la Albamu yetu na tutazunguka duniani, tunaanza na Israel hafu tuta kuwa na show pale kadhaa then tutaenda Australia tutarudi Europe tutapita nchi kadhaa, tutarudi Afrika tuna show Congo, Rwanda na nchi nyingine za Afrika then tutamaliza na Marekani”.

“Kwa hiyo Tour yetu inaanza mwezi wa Aprili mpaka Desemba ndio kitu kikubwa sana, ameongeza Nahreel.

Hata hivyo Star mwingine wa Tanzania anaeendelea na Tour yake Ughaibuni, kwama mafanikio makubwa ni Alikiba ambaye mpaka sasa ameshafanya Tour ya Afrika Kusini na Marekani na ratiba yake inaonesha ataendelea na ziara yake Barani Ulaya.
 
Top