Menu
 

Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines, limefanikiwa kukamilisha safari ya ndege iliyosimamiwa na wanawake pekee.


Ndege hiyo imetua katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.

Marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege hiyo wote walikuwa wanawake, na ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kuandaa safari kama hiyo.

 Shirika la ndege la Malawi Airlines lilianzishwa Julai 2013 baada ya kuvunjwa kwa shirika la awali la Air Malawi Februari mwaka huo. 

Chanzo:- BBC
 
Top