Menu
 
Hitmaker wa “Daffa” Pam D, afunguka kuwepo kwa wimbo wa kushirikiana baina yake na mkali wa dance na zouk rhumba Kanda Bongoman.


Sote tunafahamu fika kuwa baba mzazi wa Pam D, Shedrack Nyato ambaye sasa ni marehemu, aliwahi kuwa mpiga gitaa mahiri wa msanii huyo mkongwe mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) Kanda Bongoman.

Watarajia am, kufanya kazi na Kanda Bongoman, yah nishaongea nae nab ado kumtumia tu beat, so wakae tayari kwamba kuna kazi nafanya na Kanda Bongoman” amesikika Pam D kupitia kipindi cha The Splash kinachosikika kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa hapa redio Ebony FM.

Pam D ameongeza kuwa ukaribu wa marehemu Baba ake Mzee Nyato na Kanda Bongoman umeongeza urahisi wa kulamba bingo hiyo, ambayo huenda kila msanii amekuwa na ndoto au kutamani kuipata.

 “Yeye mwenyewe pia ni mtu ambaye ananipenda, na ameahidi kuni-support vitu vingi katika muziki wangu na pia kuna wakati huwa nawasiliana nae kwa hiyo ni kitu ambacho akaniambia nataka nikusaidie nataka kufanya kazi na wewe kwa hiyo hakuwa mgumu yeye kaona jinsi Pam alivyofight” amesema Pam D.

WATCH NEW VIDEO:- PAM D - DAFFA.
 
Top