Menu
 Chief Executive Officer wa Switch Records na Rapper mkali Bongo Quick Rocka anatarajia kuachia Albamu yake mpya msimu wa baridi au mavuno mwezi  Juni au Julai mwaka huu(2017).


 “Kuna ngoma 15 ambazo zipo tayari lakini bado naendelea kurekodi nataka albamu iwe imeshiba zaidi,  nataka kitu kitakachokuja kiwe tofauti na nyimbo ambazo zitakuwa kwenye albamu zitakuwa mpya kabisa ambazo sijaachia wala video zake” Quick Rocka amekiambia kipindi cha The Splash cha Ebony FM.

Ameongeza kuwa kwa kuzungumzia wasanii aliowashirikisha mpaka sasa na ambao anatarajia kuwashirikisha katika ngoma zitakazopatikana katika albamu yake.

 “Ni wengi mpaka sasa so far wasanii wapo wanne wakubwa na kuna wengine international ambao bado hawajarekodi lakini tushafanya nao mazungumzo na wako willing kufanya tunasubiria feedback kutoka kwenye menejimenti zao nadhani itakuwa albamu kali”.

Wakati tukiendelea kusubiria albamu hiyo, Mwezi huu Machi mwishoni Quick Rocka ataajia ngoma yake mpya kwa hiyo kaa mkao wa kufurahi na muziki mzuri.
 
Top