Menu
 

Female Rapper Rosa Ree kutokea code +255 Bongo Tanzania amekuwa ni miongoni mwa mastar wachache Afrika kuuza ngoma zao kupitia mtandao wa Tidal, unaomilikiwa na Rapper nguli kutokea Nchini Marekani Jay Z.


Up In The Air ni latest Song kutoka kwa mwanadada huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa nchini kutokana na ukali wake katika rap, akiwa chini usimamizi wa Record Label ya The Industry inayomilikiwa na Mwanamuziki na Mkali wa Midundo Bongo Nahreel.

Rosa Ree amesikika akipigia mstari na watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji, katika kipindi cha The Splash kinachosikika Ebony FM Redio, kilichopo Nyanda za Juu Kusini.

“Suala la kuweka muziki kwenye Tidal, ni suala ambalo halina ugumu wowote msanii kama msanii anapaswa kuangalia anataka kufikisha muziki wake wapi, kwa hiyo sisi kama The Industry tunataka kufikisha muziki wetu mbali zaidi”.

Ameongeza kwa kutaja tovuti nyingine ambazo wameingia nao kibiashara kwa ajili ya kuuza kazi zake  “Tukianzia na nyumbani hapa nyimbo zipo kwenye mkito, mdundo, wasafi.com kwa hiyo watu wa nyumbani wanaweza kupata na pia watu wa nje tukawa wawekea kwenye spotify, tidal, itunes na the lest of the platforms kwa hiyo wanaweza kuzipata”.

“Kwa hiyo muziki tunataka tuufikishe katika anga za juu zaidi na anga za mbali zaidi, ili watanzania tuweze kuonekana pia tunaweza na tuna vipaji na tunauwezo mkubwa katika muziki maana tidal ni platform kubwa ambayo inafikisha muziki internationally na ambao bado hawajaweza kufanya hivyo nawashauri waweze kufanya hivyo” ameongeza Rosa Ree.

Hata rapper huyo ana ndoto kubwa yakuja kufanya collabo na Rapper Jay Z…… Kila la kheri Rosa Ree Mwenyezi Mungu azidi kukupigania na kipaji chako kidumu ili uweze kutimiza ndoto zako na upeperushe bendera ya Tanzania.


 
Top