Menu
 Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake Duniani hufanika kila mwaka Machi 8, baada ya umoja wa mataifa kuianzisha rasmi mwaka 1945 kwa lengo la kutetea haki, usawa na maendeleo ya wanawake, lakini kwa Tanzania yalianza kuadhimishwa mwaka 1996.


Lakini maadhimisho hayo kwa mwaka huu yenye kauli mbiu ya  ‘Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi, imewezwa kuadhimishwa na ma – star wa kike kwa njia tofauti.

Kwa Tanzania Rappa wa kike TAMMY THE BADEST ameweza kuiadhimisha siku hii muhimu kwa kuachia ngoma iitwayo MTOTO WA KIKE, idea ya ngoma yake hii nzima anafunguka kupitia Pigia Mstari ya THE SPLASH hapa EBONY FM RADIO.

“Mtoto wa Kike ni kwaajili ya watoto wakike kote Dunia ambao wana-hustle kwa njia moja ama nyingine, wanakatishwa tamaa zile challenges wanazokutana nazo mwisho wa siku wana stickup na kuendelea kukaza” amesema Tammy.

Kwa maelezo zaidi msikilize hapa chini Tammy Akifunguka mengi zaidi.


 
Top