Menu
 Hitmaker wa Lugha Gongana Noorah yupo tayari kurudi katika gemu la Muziki wa Kizazi kipya, endapo akijitokeza mtu anayetaka kuwekeza katika muziki wake.


''Kwa hiyo kwa sasa hivi nimeamua mimi nisikurupuke, nikae kwanza nijipange niangalie kama mimi mwenyewe binafsi nitapata mtonyo wa kutosha kwamba project hii niifanyie promo au nipate mtu ambaye anaweza kuwa interested na kuwekeza au ku-finance kwa sababu kuna kazi ambazo tayari nimeshazirekodi na hata zikikaa miaka miwili bado zitafanya vizuri na kuwafikia watu kwa hiyo nataka kuwe na establishment kabisa ya kibiashara kazi zifanayika,zipushiwe na kufika zinapotakiwa kufika na mtu anayewekeza apate chake na mimi nipate changu''. amesema Noorah.

 Noorah ameelezea sababu zilizo mkatisha tamaa katika muziki ''Kuna nyimbo mbili tatu nilizitoa zilikuwa kali sana kama Chambervement niliyomshirikisha 'Marehemu Magwair' na Mapenzi Sinema niliyomshirikisha 'Dataz' hazikufika katika kiwango ambacho zilistahili kufika na hata baada ya Lugha Gongana nikatoa ngoma nyingine niliyofanya na Dully Sykes na Chege nayo haikufika katika kiwango ambacho ilistahili kufika.

''Sasa ikanifundisha kuwa muziki wa sasa hivi umebadilika tofauti na ule wa zamani wa kwamba unafanya tu ngoma unaachia halafu kwakuwa wewe ni mtu fulani utapata sapoti fulani muziki wa sasa hivi umekuwa biashara maana yake lazima mtu ujipange, ufanye promotion ya muziki wako ili watu uweze kuufikia kwa ukubwa zaidi ili uweze kufanya biashara'' ameongeza Noorah.
 
Top