Menu
 


Zikiwa zimesalia siku 21 kuachiwa kwa Albamu ya Saba ya Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva Lady Jaydee, iitwayo Woman imemfanya kuingia Chimbo na kuendelea kuisuka zaidi ili kuhakikisha mashabiki wake wanakipata kile ambacho wanakihitaji.


Albamu ya Woman ni albamu inayomwelezea mwanamke ambaye tayari ameshakua kiumri, ameshapitia vitu vingi, anaijua furaha yake, anajua sehemu yake ya kusimama katika maisha, na ngoma zitakazo patikana katika albamu hiyo sio za masikitiko sana wala sio za furaha sana.

Lady JayDee amefunguka kwa kuzungumzia Wasanii walioshirikishwa katika albamu hiyo “Sauti ambazo zitegemewe kusikika kwenye albamu hii, ni pamoja na watu kama Dj Maphorisa, Mazet, Dabo, Hamoba, Spice na wasanii wemgine wengi tofauti” amesema Lady JayDee.
Dj Maphorisa
 Hamoba
 Lady Jaydee & Spice

Kwa upande wingine ameelezea mbinu zitakazotumika kuiuza albamu hiyo yenye umuhimu mkubwa kwake.

“Mfumo ambao nitatumia kuisambaza albamu hii ni mfumo wa Internet watu ammbapo watapata ku download kutoka kwenye tovuti mbalimbali, lakini vilevile katika matamasha ambayo nitakuwa nikifanya CDs zitakuwa zikipatikana suala la kusema mtaani itakuwa inauzwa kiasi gani, sio suala ambalo nimelipanga kuuza CD mtaani kwa sababu soko hilo kiukweli lishakufa”.

Ameongeza kuwa “Kwa hiyo sehemu zile ambazo watakuwa wakisikia Lady Jaydee and The Band watakuwa na uwezo wakupata CDs, na vilevile kwenye tovuti mbalimbali ambazo tutaweza kuwatangazia watakuwa na uwezo wa ku-download moja kwa moja na kupata kusikiliza miziki hiyo, kwa hivyo kila mtu atakuwa na access ya kusikiliza”.

MSIKILIZE HAPA LADY JAYDEE AKIICHAMBUA ALBAMU KIUNDANI.
 
Top