Menu
 Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii lazima utakuwa umekutana na jambo hili linalotafsiriwa kuwepo kwa ugomvi kati ya Timu Kiba na Hitmaker wa Acha Niende Barakah The Prince.

Timu Kiba wamemtolea shutuma Barakah The Prince kuwa snitch/msaliti, amekuwa akijipendekeza kwa WCB lengo likiwa ni kutaka kujiunga nao baada ya kuonekana akiwa meza moja na mmoja wameneja wa Diamond Platnumz katika warsha moja aliyodai Barakah The Prince alialikwa na kituo kimoja wapo cha redio.

Shutuma nyingine zikidaiwa kuwa Barakah The Prince kwenye mtandao wa Kijamii wa Instagram kumu-unfollow Alikiba na kumuacha Diamond Plutnumz, tuhuma nyingine zikitajwa kuwa Barakah kasema Alikiba anapendelewa na Menejiment ya ROCKSTAR4000.

Huku Barakah The Prince yeye akiwatuhumu Team Kiba kumuendesha/kumpelekesha na kumpangia namna ya kuishi, tuhuma hizi zimesababisha kuwepo na mabishano hadi kufikia hatua ya kutukanana matusi ya nguoni na kutishiana.

Barakah The Prince amepigia mstari na kutoa msimamo wake juu ya bifu hili, wakati akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo Mbunji, wa kipindi cha The Splash kinachoruka kupitia Ebony FM Radio.

“Mimi sinaga Timu mimi timu yangu ni Yanga, sinaga timu sijui nini sijui Timu nani sijui timu nani(anasisitiza), hizi timu za watu binafsi mimi sizifahamu sizijui kabisa, Mimi namfahamu Ali kama Ali kama brother angu ni mtu ambaye nipo naye kwenye record label moja tunafanya kazi tunafanya kazi(anasisitiza)” amesema Barakah The Prince.

“Aaah Diamond pia namfahamu kama mtu wa karibu kwa hiyo mimi vitimu timu hivi(anasita), unajua huwezi kumpangia mtu namna ya kuishi au aishi na nani afanye biashara na nani au akutane na nani kwa sababu mimi mwisho wa siku nina empire yangu mimi sijawahi kusema nataka sijui Timu Barakah The Prince hata siku moja”  ameongeza Barakah.

Aidha Msanii huyo anaendelea kutetea hoja zake ili Timu Kiba wapate kuelewa ni nini anakihitaji katika maisha yake kwa sasa kupitia muziki.

“Kwa sababu mimi sitaki timu mimi nataka uwe shabiki yangu, uwe shabiki wa muziki wangu usiniingilie kwenye mambo yangu personal kwa sababu haujui pesa yangu naipata wapi na hujui nafanya nini naipata hela yangu ya muziki”.

Barakah The Prince anaendelea kusisitiza “We ni shabiki tu unataka niimbe kazi nzuri upende na u-enjoy tu ila hujui background yangu kuna nini kwa hiyo sitaki chochote sijui kuhusu timu na ukijiona shabiki wangu wakutukana tafuta msanii mwingine wakumshabikia”. 

Kwa upande mwingine anatoa ushauri kwa mashabiki wote wa muziki wa Bongo Flava. 

“Kwa hiyo kama ni shabiki yangu na mimi si msanii wa BongoFlava kwanini usifanye kuwa shabiki pia wa Diamond, kwa nini usimsapoti pia Alikiba au kwanini usimsapoti Ben Pol wewe unataka kuleta timu ili iweje? Mimi sihitaji gemu yangu haiku hivyo nafanya good music na type pia ya mashaibi zangu ukiona shabiki yoyote anatukana matusi kwenye internet huyo sio shabiki yangu sitaki mashabiki wakutukana sitaki mashabiki wapumbavu”.

Hata hivyo Barakah The Prince anafafanua zaidi aina ya mashaniki wake “Nina mashabiki watu wazima, ndio maana kwenye ma-event mpaka Bungeni wapi naitwa sometimes kwa sababu naimba muziki ambao kila mtu anaweza kuusikiliza Watoto, akina Mama, Wazee na Vijana”.

Lakini, Suala la kujiuliza ni je, nini hatima ya ugomvi huu na unatija gani katika kukuza muziki wetu wa Bongo Flava?
 
Top