Menu
 

Toka jana usiku wasanii watatu ambao ni Roma, Monii Centrozone, Bin Laden pamoja na Imma ambaye ni mfanyakazi wa Mama mzazi wa mmiliki wa studio za Tongwe Records J Murder, mpaka muda huu hawajaweza kupatikana na haifahamiki wapi walipo baada ya kuvamiwa studio na kuchukuliwa.
Muda mchache, J Murder ameeleza kiundani juu ya tukio hilo ambalo binafsi limemshtua sana, wakati akihojiwa na watangazaji Chris Bee na Fredoo kupitia kipindi cha The Splash kinachoruka redio Ebony FM.

“Sijui kisa ni nini kusema ukweli kwa sababu mimi studio sikuwepo ila kitu ninachojua mimi ni kwamba walikuja watu pale na gari aina ya Noah wakamhoji Roma baada ya hapo wakawahoji na watu wengine halafu nasikia wakaingia studio nakujukua baadhi ya vifaa” amesema J Murder.

“Baada ya hapo wakaondoka na wasanii wangu, amechukuliwa Roma, Monii, Bin Laden pamoja na mfanyakazi wa mama angu anaitwa Imma, mpaka sasa hivi hatujui wako wapi namba zao zinaita lakini hazipokelewi wakati wakivamiwa kulikuwa hakuna ulinzi walikuwepo Wsanii hao na majirani ambao ni mashabiki wa studio” ameongeza J Murder.

Mapema leo Mmiliki hiyo wa Tongwe Records alifika kituo cha Polisi Osterbay  na anaendelea kutujuza kilichomfikisha pale.

“Jana usiku baada ya kutokea tukio nilienda kutoa ripoti pale polisi Osterbay kwa hiyo leo nilichoenda pale nikujua mpelelezi wa kesi yangu ni nani nimpe maelekezo wa vitu gani vime-happen pale studio”.

“Nachowaambia mashabiki wa Tongwe, kwamba tuwaombee ndogu zetu akina Roma, Monii, Bin Laden na mfanyakazi wetu Imma wawe salama maana hatujui wako wapi, mali si tatizo tatizo ni watu wangu kwanza mali zinanunuliwa lakini huwezi kununua roho ya mtu” J Murder amemaliza kwa kusema hivyo.

 
Top