Menu
 

Ukiingia kwenye akaunti ya Mr Nay kwenye YouTube ilikowekwa video yake ya Wapo utakutana na kumekuwepo na ukosoaji wa video hiyo kuwa maudhui yake yametoka nje ya mada au kile alichokiimba katika ngoma yake.

Huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai uoga huenda umechangia nakushindwa kuitendea haki.


Mr Nay a.k.a Ney wa Mitego ametolea ufafanuzi juu ya ukosoaji huo katika kipindi cha The Splash ya Redio Ebony FM wakati akihojiwa na watangazaji wa kipindi hicho Chris Bee na Fredoo Mbuji.


“Ni video ambayo imeleta uhalisia inaleta picha ya kile ambacho nimekiimba japo kuwa hatukuweza kufanya vitu vyote lakini kwa asilimia kubwa tumevifanya” amesema Mr Nay.


“Aaaaah, ugumu ulikuwepo, ugumu ulikuwepo(anasisitiza)… ulikuwepo katika kujaribu kuweka uhalisia wa matukio hivyo ndivyo vilikuwa vinatupa ugumu kiasi fulani lakini Mungu mkubwa tumefanikisha lakini kwenye suala la ku-shoot watu sijui nini kila kitu kilikuwa ni rahisi ushirikiano ulikuwa wa kutosha uoga haukuwepo” ameongeza Mr Nay.
 
Top