Menu
 


Mkali wa Melody AT amezifungukia sababu za kuamua kugeukia katika muziki wa Bongo Flava ambao ndio ulimtambulisha vema katika Bongo Music Industry kabla ya kuukacha na kuingia katika muziki wa mduara uliomfanya kujizolea mashabiki lukuki.
 Msanii AT.


AT amesikika katika Kipindi cha The Splash akipigia mstari baada ya kuhojiwa na watangazaji wa kipindi hicho CHRIS BEE na FREDOO MBUNJI sababu zilizomfanya kuukacha muziki wa mduara.


“Mduara soko lake sio kubwa kama Bongo Flava kwa ndani, lakini mduara nje unasoko kubwa sana, lakini mduara hauna competition. Mimi nilibaki mimi kama mimi kwenye mduara hakuna watu, na watu wakitaka kuamini hicho waingie hata wasanii wafike hata 14 halafu wafanye miduara, halafu tufanye ili gemu ya mduara iendelee kuwa kubwa. Ukizungumzia mduara obvious unamzungumzia AT ” amesema AT.  


“Sasa Bongo Flava ina competition kwa sababu ina wasanii wengi, mduara haina wasanii wengi kwa hiyo hata competition inakuwa ndogo, hata ligi ianzishe wa Timu 5 na nyingine ya Timu 20 ile ya timu 20 itakuwa ligi ambayo inachangamua na watu wengi ndio wataenda kuangalia, kwa hiyo wajue Mduara haunasoko ndani lakini nje unasoko kubwa(amesisitiza)’’ ameongeza AT.


Hata hivyo AT ameendelea kusisitiza mashabiki wake kuendelea kumpa sapoti katika muziki wa Bongo Flava ambao anaamini kuwa ndio ulimpa nguvu kubwa kwa mashabiki wake kumfahamu.


Endelea Kupata burudani kwa kutazama Video mpya ya Chris Bee ft Petronia - Bashee.

Post a Comment

 
Top