Menu
 


Hitmaker wa Meremeta Nuh Mziwanda kuja na ngoma mpya aliyomshirikisha malkia wa Taarabu Khadija Kopa.

Nuh Mziwanda ambae pia ni Baba wa Mtoto mmoja aitwaye Anyagile amesikika katika kipindi cha The Splash akipigia mstari kuhusiana na miradi yake kadhaa anayotarajia kuiachia.

“Wimbo yangu mpya nimemshirikisha Khadija Kopa na nyingine nimeimba mwenyewe kwa hiyo nyimbo zipo mbili "Sandakarawe" na "Mtaa wa Kongo" kwa hiyo sijajua bado naachia wimbo gani mpaka sasa hivi” amesema Nuh Mziwanda.

“Lakini Producer Mr T Touch alisema inabidi tuzisikilize kwa umakini na tujaribu kuwashirikisha wadau tujue ngoma gani inaweza kupeleka moto ule ule wa Jike Shupa” ameongeza Nuh Mziwanda.

Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa Khadija Kopa kushirikishwa na wa sanii wa Bongo Flava, ambapo pia hivi karibuni alishirikishwa Aslay kupitia ngoma ya Usiitie Doa vilevile Diamond Platnumz kupitia ngoma ya Nasema Nawe.

Endelea Kupata burudani kwa kutazama Video mpya ya Chris Bee ft Petronia - Bashee.

Post a Comment

 
Top