Menu
 

Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Nchini Tanzania Flora Mbasha akanusha taarifa za Utata zilizozagaa mitandaoni kuwa "Haina haja zakuwa na Mwanaume ambae hakuridhishi kinyumba"
 
Kupitia akounti yake ya Instagram @flora_madam amechapisha ujumbe huu "Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na radio yoyote na kuzungumza maneno hayo kama ilivyo sambaa mitandaoni. Naomba mzipuuze maana ni mpuuzi mmoja tu ameamwua kuonyesha upuuzi wake na kutafuta followers kwenye page yake".

Licha ya ufafanuzi huo lakini hachasita kutoa onyo kwa waandishi wa stori hiyo. "Na niseme tu kwamba hivi sasa sitakaa kimya tena, huyo aliyezoea kunizushia story za uongo akifikiri siijui sheria ajipange vizuri maana mahakama ipo na sheria ipo".

Narudia tena kusema "HABARI HII ILIYOSAMBAA MITANDAONI NI YA UONGO SIJAZUNGUMZA MIMI MANENO HAYO" Kitabu ndio kimetoka last wk cha "SIRI ZA FLORA MBASHA" lakini sijafanya interview yoyote na kuongea upuuzi huo kama ilivyosambaa.

Post a Comment

 
Top