Menu
 

Mwanamuziki nguli wa Bongo Flava Alikiba na Music Label ya Rockstar4000 wametangaza kusaini makubaliano ya pande zote mbili/Partnership ya umiliki wa #ROCKSTAR4000 hiyo ikimaanisha Alikiba kwa sasa atakuwa katika Bord ya Wakurugenzi ana (Hisa) shares katika #ROCKSTAR4000.
.
Habari njema kupitia makubaliano hayo, yanamfanya kuwa mmoja wa Wamiliki pia wa TV #RockstarTV ambayo hufanya kurusha Taarifa zake za kiburudani kupitia Tv mbalimbali ilizoingia nazo mkataba kama #MTN ya South Afrika.
.
MENGINEYO: hii ni kutokana na Maswali mbalimbali yaliyoulizwa:-.
1.Nyimbo Mpya:- Alikiba aligusia inatoka wakati wowote, inafanyiwa marekebisho tu na Director katika upande wa video kama ni ng'ombe kumla basi kabakia mkia.

2.International Collabo Zipo na zitakujia kwa sababu kasikika pekee yake kwa muda mrefu.

3. Media Tour West Africa; Mipango ipo nailishaanza kufanyika. 

4. Album(Diary of Alikiba):- Ipo inaandaliwa iko kwenye kukamilika na itauzwa kwenye Digital stores zote iTunes,Spotify n.k 

5.Kashfa ya kukataa Mtoto Mombasa nakupelekea Mwanamke kutua Bongo- Vitu kama hivyo vyakusingiziwa vipo sana kwa Mwanaume Rijali.

6.Show za Fungamwaka na KINGKIBA:- Itakuwepo na itahusisha Wasanii wengi tu na itafika hadi mikoani.

7.Announcements zimeisha?:- Akadai Bado zingine kibao hata kesho(leo) inaweza kuwepo kwa sababu kuna mambo kibao ambayo yamempeleka Afrika Kusini.

Post a Comment

 
Top