Menu
 

TIMBULO ni miongoni mwa wasanii anzuani, si kipaji pekee alichonacho bali hata nidhamu na heshima anayoionesha kwa watu wa aina au hali yoyote na media media tofauti pasipo kuweka matabaka ndio siri pekee inayomfanya kila kazi akiitoa kupokelewa vema na kupendwa pia.
 

Sahau kitendo chake chakuachia ngona mfululizo kama Usisahau, Mfuasi, Ndotoni na hii aliyoiachia sasa Mshumaa utagundua ana utajiri mkubwa wa utunzi, maneno adhimu na melody tamu na vyote hivi ameweza kuviapply na kukonga mashabiki wake tofauti.

Miaka ya nyuma nilishawahi kufanya nae kazi katika Tour zake kadhaa ikiwemo ile aliyokuwa ameifanya nyumbani kwao Ruiwa Jijini Mbeya, niliona nna anavyokubalika sana nyumbani kwao licha ya usemi wa wahenga kuwa nabii hakubaliki kwao lakini nikahisi wahenga wakati mwingine misemo yao inatuchuuza.

Hivi karibuni kama kioo cha jamii akaona si haba kulipeleka fungu la kumi nyumbani kwao kwa kutoa misaada kadhaa kwa watu wenye mahitaji tofauti wakiwemo wazee, wagonjwa na hata wanafunzi ni hazina kubwa na baraka ambazo ataendelea kuzipata kwa jamii ile na kupata wepesi katika kazi zake kuendelea kupenya.

Hii inawakumbusha hata wasanii wengine kurudi kwa walaji wa kazi zao ambao ndio mashabiki na wanaowafanya wawepo mpaka sasa kwenye mainstream, kuacha dharau, kujisikia na kusahau walikotoka hii ni mbaya sana kwa sababu wakishasuswa na fans wao hujihisi wamepata mkosi kumbe ni matokeo ya tabia zao zisizompendeza kila mtu.

TIMBULO ni miongoni mwa wasanii ambao waliathiriwa sana na scandal ya kucopy nyimbo za X MALEYA kutoka Cameroon nakupelekea mshabiki wake kukosa imani nae na kila alivyokuwa akitoa kazi zilikuwa hazipokelewi vema licha ya ukali na ubunifu japo hata figisu figisu kadhaa za wapinzani wake zilichangia.

Lakini hakukata tamaa aliingia chimbo na kuangalia njia mbadala yakurejesha heshima kwa mashabiki wake waliokosa imani nae na namna yakuzikabili figisu figisu zinazomkabili na namna gemu la muziki linavyobadilika na akafanikiwa kurudi na coming back yake imekuwa tishio sana.

Mwisho Timbulo ni msanii wakuangaliwa sana sana na naamini ni moja ya wasanii wakuangaliwa sana endapo hatokumbwa tena na visa vingine vya figisu figisu.

Post a Comment

CHRIS BEE TZ said... 7 July 2017 at 13:26

Big up kwake nidham ndo mwanga wa mafanikio popote duniani.

 
Top